Jumanne 15 Septemba 2026 - 12:20
Hashd al-Shaabi ni nguzo kuu ya usalama wa eneo

Hawzah/ Rabii Soran, mjumbe wa Baraza la Mkoa wa Nineveh kutoka katika jamii ya Wakristo, amesisitiza kwamba; silaha kuwa chini ya mamlaka ya serikali hakumaanishi kwa namna yoyote kuvunjwa au kusambaratishwa Hashd al-Shaabi.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Rabii Soran, mjumbe wa Baraza la Mkoa wa Nineveh kutoka katika jamii ya Wakristo, katika mahojiano maalumu na tovuti ya habari ya Al-Ahd, amesisitiza kwamba; silaha kuwepo chini ya mamlaka ya serikali hakumaanishi kwa namna yoyote kuvunjwa kwa Hashd al-Shaabi.

Amesema: “Uthabiti wa Mkoa wa Nineveh unategemea uratibu wa hali ya juu kati ya Hashd al-Shaabi na vikosi vya usalama vilivyo chini ya uongozi wa Amiri Mkuu wa Majeshi ya Iraq.”

Soran amesema: “Kwa hakika tunaunga mkono silaha zote ziwe chini ya mamlaka ya serikali na vikosi vyote viwe chini ya amri ya Amiri Mkuu wa Majeshi, lakini jambo hili kwa namna yoyote halimaanishi kuvunjwa kwa Hashd al-Shaabi wala kutoa fursa nyingine kwa mipango ya kigaidi ambayo wakati wa matukio ya mwaka 2014 ilijaribu kuliteka eneo hili.”

Ameongeza: “Hashd al-Shaabi imethibitisha ufanisi wake mkubwa katika mapigano na katika kuyakomboa maeneo, sambamba na mashujaa wa Jeshi la Iraq na taasisi za usalama katika ngazi zake zote. Leo hii, inaunda kikosi rasmi cha kijeshi miongoni mwa safu za Majeshi ya Iraq.”

Mjumbe huyo wa Baraza la Mkoa ameashiria kuwepo kwa ridhaa kubwa miongoni mwa wananchi wa Nineveh, hususan katika maeneo yanayoishi jamii za asili za Wakristo, Washabaki, Wakakai na Waizidi, pamoja na Waarabu katika makundi yao yote, kutokana na hali kubwa na inayoonekana wazi ya utulivu wa kiusalama.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha